Serikali ya kaunti ya Narok imewataka wananchi wanaopakana na msitu wa Mau kuchukua tahadhari kutokana na moto ambao umekua ukiteketeza sehemu kubwa ya msitu huo kuanzia siku ya Alhamisi ya tarehe 2 mwezi huu.

Katika taarifa iliyochapishwa alasiri ya leo na mkurugenzi wa mawasiliano kutoka katika ofisi ya gavana, moto huo umekuwa ukitoa changamoto kwa maafisa wa kuzima moto kutoka kaunti tofauti, ila ameeleza kuwa juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda, hasa baada ya kushuhudiwa kwa kipindi cha mvua katika sehemu za msitu huo.

Taarifa iliyochapishwa imeweka bayana kwmaba moti huo ilianzia katika eneo la Chebitet kabla ya kuenea katika maeneo mengine.

February 7, 2023