Waziri wa mashauriano ya nchi za nje Alfred Mutua, ametuma ujumbe wa pole kwa taifa la Uturuki linalokumbwa na jinamizi la matetemeko ya Ardhi yaliyosababisha vifo vya watu wapatao 5000 katika taifa hilo.

Katika taarifa yake aliyoitoa wakiwa na Balozi wa Uturuki humu nchini Subutay Yuksel, Waziri Mutua amewarai wakenya kuungana na wananchi wa taifa hilo na kuwasaidia kurejea katika maisha yao ya kawaida, kwa kutoa msaada wowote walio nao.

Aidha waziri Mutua ameahidi kuwa serikali imeweka mikakati ya kutoa msaada wake kwa walioathirika na mkasa huo. Hapo awali Rais William Ruto alituma ujumbe sawia kwa wananchi wa taifa hilo.

SOMA PIA |

Kenya Itasimama na Uturuki wakati huu mgumu.

Tetemeko la ardhi lililokuwa na nguvu ya 7.7 katika kipimo cha Richter hapo jana liliikumba sehemu ya kusini mashariki mwa Uturuki inayopakana na Syria. Tetemeko lingine la kipimo cha 7.5 lilifuatia wakati wa mchana.  Kwa mujibu wa mamlaka ya kukabiliana na maafa mitetemeko mingine 243 ilifuatia. Nchini Syria idadi ya watu waliokufa imeongezeka na kufikia watu 1,602 hadi sasa.

 

February 7, 2023