Rais William Ruto amesema Kenya inasimama pamoja na Uturuki na Syria kufuatia tetemeko kubwa la ardhi ambalo liliporomosha majengo na kusababisha zaidi ya watu 5,000 kupoteza maisha  huku 20,000 wakijeruhiwa.

Waokoaji wanaendelea kuwatafuta manusura kwenye vifusi vya maelfu ya majengo yaliyoporomoka kufuatia tetemeko la ardhi nchini Uturuki na Syria.

Nchi mbalimbali kote ulimwenguni zimepeleka vikosi vya kusaidia katika juhudi za uokozi huku shirika la Uturuki la kushughulikia majanga likisema Zaidi ya wahudumu 24,400 wako katika maeneo yaliyoathirika.

Aidha kutokana na ukubwa wa eneo lilioathirika ambapo takriban majumba 6,000 yaliporomoka nchini Uturuki pekee, juhudi zao ni ndogo mno.

Meli ya jeshi la wanamaji imetia nanga katika bandari ya Iskenderun, ambako hospitali iliporomoka, ili kuwasafirisha walionusurika hadi mji uliokaribu wa Mersin.

February 7, 2023