BY ISAYA BURUGU,31ST AUG 2023-Kampuni ya Kusambaza Umeme Nchini (KPLC) kwa mara nyingine imetangaza kukatizwa kwa umeme ambako kumepangwa kufanyika leo Alhamisi.

Maeneo kadhaa katika takriban kaunti saba nchini  yatakosa umeme kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa kumi na moja jioni.

Kaunti zitakazoathirika ni pamoja na Machakos, Nakuru, Elgeyo Marakwet, Kisii, Kiambu, Kilifi na Mombasa.Katika kaunti ya Machakos, sehemu za eneo la Katani zitaathirika.

Maeneo hayo ni pamoja na; Rhombus, Bluestone, Suraya, National Concrete, Veevee, Aristocrats, Kirinyaga, Mugoya, Garuda, Greatwall Gardens Phase 3, St. Franciscan Sisters, Whistling Moran’s, Harvest International, Waridi, Pine City, Nova Pioneer School, Seyani Brothers, Welding Aloys, Alrabia, Riverpark Estate, Graceland Estate na majirani zake.

Maeneo ya Kirigiti, Migaa na Toll Station katika kaunti ya Kiambu pia yataathirika. Maeneo ambayo hayatakuwa na stima ni pamoja na; Kirigiti, Riabai, Mboi Kamiti, Migaa, St. Anne’s Lioki, Karia, Todas Bar, Waironjo, Ngurunga Farm, Kifisha Farm, Nyara, Kianjimbi, Marion Sch, Shawazi, Gulmerg na vitongoji vyake.

 

Share the love
August 31, 2023