Mkurugenzi mteule wa mashataka ya umma Renson Mulele amehojiwa hii leo na kamati ya sheria katika bunge la kitaifa.

Mulele alitakiwa kueleza sababu halisi za kuondolewa kwa kesi za watu mashuhuri nchini mahakamani.

Mulele aliyehudumu katika ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kwa muda wa miaka tisa vilevile alitakiwa kueleza uwezo wake wa kuweza kustahimili shinikizo la kuchukua maamuzi ya kisiasa endapo ataidhinishwa kuchukua wadhfa huo.

Mulele aliteuliwa na rais William Ruto kuchukua nafasi ya Noordin Haji.

Share the love
August 31, 2023