Mwanasheria mkuu Justin Muturi ameapishwa kama kamishna wa tume ya huduma kwa mahakama JSC. Hafla hiyo iliongozwa na jaji mkuu Martha Koome katika jengo la mahakama ya juu. Akizungumza baada ya kuapishwa, Muturi ameahidi kuiunga mkono tume hiyo sawa na kufanya kazi kwa karibu kuhakikisha kuwa katiba na demokrasia zinalindwa.

Muturi ambaye alihudumu kama spika wa bunge la kitaifa, alitwaa rasmi wadhfa huo wa mwanasheria mkuu tarehe 27 mwezi jana baada ya kuapishwa. Muturi atawakilisha na kutoa usahauri wa sheria katika serikali ya rais William Ruto.

Naye Bi. Koome amesema ana uhakika kuwa Muturi atakuwa kamishna muhimu katika tume hiyo kwani atatumika kama kiungo kati ya JSC na serikali kuu.

November 1, 2022