Kamishana wa kaunti ya Narok Isaac Masinde amewataka wanafunzi kufanya bidii kwenye masomo yao na kuwatii walimu pamoja na wazazi wao.

Akizungumza alipokuwa akipokea ufadhili kutoka kwa wakfu wa Jomo Kenyatta Masinde amesema wanafunzi wapatao 67 kutoka kaunti hii ya Narok wamenufaika na ufadhili huo.

Aidha amewataka wanafunzi kuepuka mila potovu hasa ukeketaji na ndoa za mapema ambayo amesema imechangia kudorora kwa elimu ya mtoto wa kike.

Kauli yake imeungwa mkono na wazazi kutoka sehemu mbali mbali kaunti ya Narok wakisema hatua hiyo itainua elimu hasa katika familia maskini.

February 20, 2023