BY ISAYA BURUGU 20TH  FEB 2023-Biwi la simamzi limekumba eneo la ting’a Eneo bunge la mugirango magharibi kaunti ya Nyamira baada ya mwalimu mmoja kujiua kutokana na madai ya kulaghaiwa shilingi milioni moja unusu.

Josec Ondere mwenye umri wa miaka 38 alikuwa mwalimu katika shule ya mesto ya Gesure. Anaidaiwa ukujirusha kwenye kidimbwi cha maji eneo hilo.

Kulingana na barua aliyoandika marehemu,mwanamke mmoja alikuwa amemwandikia jumbe za kumtishia.

Aidha analalamikia kulaghaiwa na watu wengine watano shilingi milioni 1 unusu ambazo alikuwa amelipa ili kumiliki kipande cha ardhi.,aafisa wa polisi kutoka kituo cha manga Sengera walifika eneo la mkasa na kupeleka mwili wa marehemu kwenye hifadhi ya maiti.

 

 

February 20, 2023