Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki nchini (KCCB) linaitaka Mahakama ya upeo kubatilisha uamuzi ulioruhusu usajili wa vikundi vya watu wanaoendeleza mapenzi ya jinsia moja almaarufu LGBTQ.

Katika taarifa iliyochapishwa na KCCB adhuhuri ya leo, uamuzi wa kufungua mlango wa usajili kwa watu wa kundi hili ni kinyume cha katiba ya taifa la Kenya na pia Kinyume cha maadili ya taifa la Kenya. Katika taarifa yao, baraza hilo chini ya uongozi wa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Mombasa Martin Kivuva, limewataka wanyeya kusimama kidete kupinga uenezaji wa ushoga kwani unalenga kuharibu maadili ya familia na heshima ya Kikristo.

KCCB pia imeyarai mashirika mengine kujitokeza na kutoa sauti zao ili kushinikiza kuangaziwa upya kwa uamuzi huo.

March 10, 2023