Aliyekuwa mbunge wa Narok Kaskazini Moitalel Ole Kenta, hatimaye amevunja kimya chake kuhusiana na sheria mpya za usimamizi wa Mbuga ya Maasai mara, akisema kwamba uamuzi wa kutaka kuleta usimamizi mpya ni mpango unaonuia kuwafaidi wachache na wala sio kwa manufaa ya jamii.

Kenta ambaye aliwania ugavana Kaunti ya Narok kwa tiketi ya chama cha ODM katika uchaguzi wa Mwaka jana bila mafanikio, alikuwa kiwahutubia wananchi wa eneo la Nkareta, na amemsuta gavana wa sasa wa kaunti ya Narok Patric Ntutu kwa kuharakisha mchakato wa kuidhinisha sheri hizo.

Mwanasiasa huyo ameongeza kwamba lazima mbuga ya Maasai Mara ilindwe ipasavyo, kwani ni mojawapo ya rasilimali muhimu za jamii ya Maa, akiahidi kupinga mipango ya kuendelea kuhitilafiana na mbuga hiyo.

Kuhusiana na suala la Msitu wa Mau, Mbunge huyo wa zamani amemtaka Kiongozi wa Taifa Rais William Ruto Kushughulikia mizozo ya moto ya mara kwa mara katika msitu huo, kieleza kwamba mikasa hii ni mojawapo ya njia zinazotumiwa na wananchi ili kujitwalia umiliki wa ardhi ya msitu.

 

SAUTI: Aliyekuwa mbunge wa Narok Kaskazini Moitalel Ole Kenta

February 23, 2023