Idadi kubwa ya wanafunzi waliokamilisha darasa la nane mwaka jana katika kaunti hii ya Narok wamejiunga na shule za upili. Haya ni kwa mujibu wa kaunti kamisha wa Narok Isaac Masinde.
Akizungumza mjini Narok Bw. Masinde amesema tayari asilimia 80 ya wanafunzi walioandika mtihani wa KCPE mwaka jana wako shuleni kuendeleza masomo yao ya sekondari.
Aidha amewapongeza wazazi kwa juhudi walizofanya kuhakikisha kuwa wana wao wanaenda shuleni licha ya changamoto wanazopitia.