Taifa la Kenya limeungana na ulimwengu hii leo ili kuadhimisha mwanzo wa siku kumi na sita za kampeni dhidi ya dhulma za kijinsia.

Takwimu za umoja wa mataifa kuhusiana na dhuluma za kijinsia zinaashiria kuwa kati ya kila wanawake 3, angalu mmoja huathiriwa kwa njia moja au nyingine na dhuluma hizi.

Humu nchini visa vya dhulma za kijinsia vinaendelea kushuhudiwa kila kuchao huku wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wakiendelea kukaza kamba katika juhudi za kumaliza kabisa dhulma hizi. Maadhimisho ya mwaka huu yameanza rasmi hii leo na yanatarajiwa kuendelea kwa siku 16 zijazo, kutoa hamasisho dhidi ya dhuluma hizi, Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni “Tuungane tokemeshe ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.”

November 25, 2022