BY  ISAYA BURUGU ,26TH NOV 2022-Abiria 21 waliokuwa wameabiri bus la kampuni ya Gaurdian kule kisii  wamepoa kifo baada ya basi hilo kuanguka mtoni.

Hata hivyo abiria wote wameokolewa  na kupelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya kisii baada ya kupata majeraha.Basi hilo limeanguka kwenye mto nyabera kaunti hiyo ya Kisii.

Kwa mjibu wa walioshuhudia ni kwamba basi hilo limegongwa na lori la mchanga kutoka nyuma kwani lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi.

Kwa bahati nzuri mto huo haukuwa na maji mengi. wakati wa ajali hiyo basi lenyewe lilikuwa na kontakta na dereva Pamoja na abiria wengine.

 

November 26, 2022