Huku Siku ya Kifua Kikuu ikiadhimishwa duniani kote, Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kupanua wigo wa Mpango wa Kimataifa wa Mkurugenzi Mkuu wa WHO kuhusu kifua kikuu katika kipindi cha miaka minne ijayo.

Mpango huu bora unakusudiwa kusaidia maendeleo ya haraka ya kukomesha TB na kuafikia leongo la Huduma ya Afya kwa Wote UHC ifikapo mwaka wa 2030.

Siku ya Kifua Kikuu Duniani mwaka huu inaadhimishwa chini ya kaulimbiu ‘Ndiyo! Tunaweza kukomesha TB!’ kwa lengo la kukuza matumaini na kukuza uongozi wa ngazi ya juu, kuongezeka kwa uwekezaji, kupitishwa kwa haraka kwa mapendekezo mapya ya WHO, na kuimarisha ushirikiano wa sekta mbalimbali ili kukabiliana na janga la TB.

Kifua kikuu kinasalia kuwa moja ya magonjwa hatari duniani ambapo husababisha vifo milioni 1.6 kila mwaka.Kifua kikuu husababishwa na bakteria Mycobacterium tuberculosis ambayo mara nyingi huathiri mapafu.

March 24, 2023