Watu 3 wameaga dunia huku wengine 6 wakiachwa na majeraha baada ya kuhusika katika ajali ya bara barani eneo la Kisiriri kwenye bara bara kuu ya Narok-Nakuru asubuhi ya leo.

Kamanda wa polisi Narok ya kati John Momanyi ambaye alidhibitisha tukio hilo, alieleza kwamba ajali hiyo ilihusisha gari aina ya matatu na ilitokea baada ya gari hilo ambalo lilikuwa linatoka Narok kwenda Nakuru kupasuka magurudumu 2 na kubingiria mara kadhaa kabla ya kusimama. watu 3 waliaga dunia papo hapo, 3 wakaachwa na majeraha mabaya huku wengine 3 wakiachwa na majeraha madogo.

Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali ya rufaa mjini narok kwa Matibabu, huku miili ya walioaga pia ikihifadhiwa katika makafani ya hospitali hiyo. kamanda huyo wa polisi aidha alitoa rai kwa madereva kuhakikisha kwamba wanatilia mkazo sheria za trafiki wanapokuwa barabarani.

February 28, 2023