By Isaya Burugu,Oct 13,2022-Kenya imeungana na uliwmwengu leo kuadhimisha siku ya kuona .Ni siku inayoadhimishwa wiki ya pili ya mwezi Oktoba.

Kama sehemu ya maadhimisho hayo,Madakitari wa macho wamefika katika stendi ya magari mjini Kisiii kuweza kuwahamazisha madereva na wahudumu wa magari kuhusu umuhimu wa kulinda afya ya macho yao .

Pia wametoa huduma za bure za matibabu kwa wauhudumu hao sawa na ukaguzi wa macho bila malipo.Mwaka huu chama cha madkitari wa macho kinawalenga madereva wwa magari ya uchukuzi wa umma kwa lengo la kubaini kinachosabbaisha ajali kwani afya ya macho kwa madereva hao ni muhimu.

Kwa jibu wa  Dakita Daniel Mochere anayesimamia chama cha madakitari wa macho nchini ni kwamba wanalenga kupata data ya kutosha kutoka kwa kundi hilo la watu ili kufanya maamuzi muhiu kuhusu utoaji huduma bora kwao na kwa wannachi kwa jumla.

October 13, 2022