BY ISAYA BURUGU ,OCT 13,2022-Mahakama kuu imetupilia mbali, kesi ya kuharibia jina iliyokuwa iiliyowasilishwa mahakamani na kampnuni ya maziwa ya Brookside Dairy limited dhidi ya mbunge wa Nyali Mohamed Ali.
Jaji  Hedwig Ongudi amesema kuwa kesi hiyo iliyokuwa imewasilishwa mbele ya kitengo cha katiba  inapaswa kuwasilishwa kwenye kitengo kinachostahili cha mahakama.

Katika kesi hiyo  Brookside ilikuwa imemshtaki Mohamed Ali kwa kudaiwa kuwachochea wananchi  ili kuadhiri kiuchumi na kibiashara shughuli za kampuni hiyo.

upande wake Ali aliwasilisha pingamizi akisema kuwa kuna haki zake msingi ambazo zimekiukwa na akaitaka mahakama kufutilia mbali kesi hiyo.

Mbunge huyo kupitia wakili wake Adrian Kamotho  alikuwa amedai kuwa  nguzu za mahakama zilikuwa zimetumiwa visivyo kwani hatua ya kuendeleza kesi hiyo ni kinyume cha matarajio ikizingatiwa kuwa brookside ni kampuni ya kibinafsi.Kesi hiyo imetupiliwa mbali.

 

 

October 13, 2022