Naibu wa Rais Rigathi Gachagua ameahidi kuwa wakenya hawatakua na haja ya kuhofu kuhusu kufurushwa makwao kiholela au kubomolewa makaazi yao nyakati za usiku.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa shule ya Komarok jijini Nairobi alikoandamana na Rais William Ruto, Gachagua amesema kwamba serikali ya Rais William Ruto imetoa ilani kwa viongozi wote watakaotekeleza maagizo yoyote ya kuwafurusha wananchi kutoka kwa makaazi yao pasi na kujadiliana na idara za usalama katika kaunti husika. Naibu wa rais amesisitiza wakenya watakao furushwa kutoka katika ardhi ambayo si yao watapata maeneo mbadala watakapoishi.