Kenya imeungana na ulimwengu hii leo kuadhimisha siku ya walemavu duniani kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa Suluhu za mageuzi kwa maendeleo jumuishi.

Kaunti ya Narok vilevile haijaachwa nyuma katika kuadhimisha siku hii ambapo hafla ya kuwasherehekea watu wenye ulemavu iliandaliwa katika uga wa Ole Ntimama.

Hafla hiyo iliongozwa na gavana wa kaunti hii Patrick Ntutu.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ntutu ameahidi kuzingatia maslahi ya walemavu katika kaunti hii sawa na kutekeleza matakwa yao.

Kwa upande wake waziri wa leba bi Florence Bore ambaye alikuwa mgeni mheshimiwa amedokeza kuwa serikali imetenga fedha ambazo zitawasaidia watu wenye ulemavu kujikimu kimaisha huku akiweka wazi  watu wenye ulemavu ambao wamehitimu katika kozi mbalimbali watapata nafasi za ajira.

Naye kamishna wa kaunti hii Isaac Masinde ameahidi wataendelea kushirikiana na baraza la watu wenye ulemavu katika kaunti hii ili kuhakikisha kuwa haki zao zinalindwa.

Hali kadhalika mmoja wa wawakilishi wa walmavu katika kaunti hii ya Narok ameitaka serikali ya kaunti kuwatengea nafasi katika bunge ya kaunti ili waweze kuwasilisha matakwa yao.

 

December 3, 2022