BY ISAYA BURUGU 5TH DEC,2022-Wiliam Ruto amesema kuwa  kuna haja ya kukumbatia mifumo mengine ya kutafuta haki badili ya kutegemea mahakama pekee.Akizungumza jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa tume ya utekelezaji sheria na idara ya mahakama,Ruto amesema kuwa kwa sasa mahakama za humu nchini zinakumbwa na changamoto mbali mbali zikiwemo kusanyiko wa kesi hali ambayo inaweza badilika iwapo wahusika watakumbatia mifumo mbadala ya kusaka haki.Rais pia amedokeza kuwa hakuna yeyote atakayekwepa kulipa kodi na kutumia mahakama kujilinda kwa makosa hayo.Aidha ameahidi kuwa serikali yake itaiunga mkono kikamilifu idara ya mahakama katika kutekeleza jukumu lake ambalo amesema ni muhimu kwa uongozi wa nchi.

Mungano wa ulaya ambao umewakilishwa katika kongamano hilo umeitaka serikali kuhakikisha kuwa inaondoa vikwazo vyovyote vinaleta vizingiti katika kuwapa haki wananchi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa mashataka ya umma Noordin Haji anasema afiis yake inandaa mswada utakaofafanua jukumu la kila mhusika katika mchakato wa utekelezaji haki ili kuepusha mgwaruzano ambao umekuwa ukishuhudiwa baina yao.

Kongamano hilo limehudhuriwa na wahusika mbali mbali kwenye mchakato mzima wa utekelezaji sheria.

 

December 5, 2022