Aliyekuwa katibu katika wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho, ameikabidhi mikoba ya wadhifa huo kwa katibu mpya Raymond Omollo ambaye anatarajiwa kuanza jukumu lake katka wizara hiyo baada ya kuapishwa kwamo mwishoni mwa wiki iliyokamilika.

Akizungumza baada ya kutwaa ofisi yake rasmi, Omollo amesema kuwa atafungua milango yake wazi ili kuweza kuwahudumia wakenya na kuwapa huduma wanazohitaji kwa njia mwafaka.

Kibicho kwa upande wake ameahidi ushirikiano wake na katibu mpya wakati wowote atakapohitaji.

December 5, 2022