BY ISAYA BURUGU ,6TH DEC 2022-Shirika lisilokuwa lakiserikali linalojihusisha na upanzi wa miti la pafeed limezindua  mradi wa upanzi wa miti katika shule ya msingi ya  Nairasirasa kaunti ya Narok.Kufikia sasa limepanda jumla ya miti 3900 katika maeneo matatu tofauti.

Kulingana na Charles morompi ambaye ni mfanyikazi katika shirika hilo anasema kuwa wanajihuisha na utoaji mafunzo kwa wakulima jinsi ya kutunza udongo na kuhakikisha unasalia katika hali nzuri kila mwaka wakati wa msimu wa upanzi.

.Aidha  amewahimiza wakulima kutochoma mabaki ya vyakula  kwani mabaki hayo ndio mbolea inayoipa mimea rotuba mimea. .Kwa upande wake mzee wa Kijiji katika eneo hilo Daniel olendogoyua anasema kuwa mafunzo waliopokea yatawafaa kwa kiwango kikubwa na wana Imani wataimarisha mazao yao katika misimu ijayo.

Shirika la Pafeed limefadhiliwa na  ,shirika la world food programme katika kufanikisha mafunzo hayo.

 

 

 

 

December 6, 2022