Viongozi wa upinzani wakiongozwa Raila Odinga na Martha Karua ambaye ni kinara wa chama cha Narc Kenya, wataandaa hafla yao ya maadhimisho ya sherehe za Jamhuri, kando na ile itakayoandaliwa na kuongozwa na rais William Ruto.

Karua ambaye aliiwasilisha taarifa ya muungano huo alasiri ya leo, ameweka wazi kuwa hafla yao itaandaliwa katika uga wa Jacaranda jijini Nairobi. Viongozi hao aidha wamesisitiza kwa mara nyingine kuwa wako tayari kutetea haki za wakenya kwa kuishiurutisha serikai kufuata sheria katika utendakazi wake.

Kuhusiana na maswala ya maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumatano, Karua amesisistiza kuwa maandamano hayo yatakua ya amani, akitupilia mbali semi za Rais na naibu wake kuwa mali ya wananchi yataibiwa au kuharibiwa wakati wa maandamano hayo, na badala yake wakusuta uongozi wa Rais Ruto kama unaochukua mkondo wa kibepari.

December 5, 2022