Rais William Ruto ametuma onyo kali kwa wananchi waliokuwa na hulka ya kukwepa kulipa ushuru nchini.

Akizungumza kutwa ya leo alipohudhuria semina ya baada ya uchaguzi iliyoandaliwa wa ajili ya wabunge katika kaunti ya Mombasa, Rais Ruto amewakemea wapinzani wake waliowataka wafuasi wao kutolipa ushuru wakisema kuwa ushuru unaokusanywa sio wa haki, badala yake rais amesema kuwa hakua jambo litakalowaficha au kuwaepusha na ulipaji wa ushuru kwa vyovyote vile.

Matamshi ya Rais yamekujia siku moja baada ya semi za kinara wa muungano wa Azimio la Umoja Raila Odinga, katika mkutano wa hadhara na wafuasi wake katika ua wa Jacaranda, kuwataka wafuasi wake kutolipa ushuru, kwa kigezo kuwa ushuru unaokusanywa nchini ni wa kuwadhulumu.

Rais ameeleza kuwa maandamano yanayoshuhudiwa ni njia ya baadhi ya viongozi kukwepa ulipaji wa ushuru, jambo ambalo ameahidi kuwa halitakubalika wakati wa uongozi wake.

January 30, 2023