Rais William Ruto amepuuza tetesi za mkutano kati yake na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya IEBC Wafula Chebukati kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa kongamano la muungano wa viongozi wa mashtaka katika kaunti ya Mombasa, Ruto amepuuzilia mbali madai hayo yaliyotolewa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga katika uwanja wa Jacaranda hapo jana.

Aidha amehoji sababu ya masuala hayo kuibuka wakati huu ilhali upande wa upinzani ulikuwa na fursa ya kuwasilisha ushahidi wao wakati wa kusikilizwa kwa kesi ya uchaguzi.

Hali kadhalika rais ameahidi kutekeleza ahadi ya serikali ya kutenga rasilimali za kutosha ili kuwezesha taasisi mbalimbali kwenye idara ya utawala, haki, sheria, miongoni mwa mambo mengine, kufanya kazi zao kwa ufanisi.

 

January 30, 2023