Waziri wa usalama wa ndani nchini Kithure Kindiki amezindua kikosi maalum kitakachosaidia kupambana na uhalifu katika sekta ya usambazaji na uhifadhi wa maji nchini, huku pia akiwaonya wanaoharibu miundomisingi ya maji kuwa chuma chao ki motoni.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Waziri Kindiki amekiri kuwa wizi na uharibifu wa vifaa na mitambo ya maji umekithiri humu nchini, jambo lililosabaisha kuzinduliwa kwa kikosi maalum cha maji almaarufu Water Police Unit au WPU kilicho ndani ya kiosi cha polisi wa utawala.

Wizara ya maji imesema kuwa imepoteza shilingi bilioni 10 kupitia wizi na uharibifu wa mitambo yao katika maeneo mbalimbali yataifa

January 30, 2023