Kiongozi wa upinzani Raila Odinga sasa anataka kujiuzulu mara moja kwa Waziri wa Kawi Davis Chirchir na mwenzake wa Hazina ya kitaifa Njuguna Ndung’u.

Hii ni kutokana na madai ya mpango wa ununuzi wa mafuta kupitia mkataba uliotiwa saini kati ya serikali ya Kenya, Saudi Arabia na UAE.Odinga anadai kuwa mkataba huo ulitiwa saini na kuwekwa siri ili kuongeza gharama ya mafuta nchini.

Aidha alisema kuwa Kenya haikutia saini mkataba wowote na UAE au Saudi Arabia na kwamba mkataba huo ulitiwa saini kati ya Wizara ya Nishati na kampuni zinazomilikiwa na serikali katika eneo la Mashariki ya Kati.

Akihutubia wanahabari jijini Nairobi, Odinga aliwashutumu Chirchir na Ndung’u kwa kutekeleza uhalifu na kusema ni lazima waondoke afisini na kufunguliwa mashtaka.

&nbs

p;

Share the love
November 20, 2023