BY ISAYA BURUGU 5TH DEC 2022-Naibu mwenyekiti wa tume ya IEBC Juliana Cherera amejiuzulu kwenye wadhifa wake katika tume hiyo.Katika barua yake kwa rais William Ruto, Cherera alimjulisha kuhusu kujiuzulu kwake kutoka kwa baraza hilo la  uchaguzi.

Cherera alisema katika kipindi chake kama kamishna alitekeleza majukumu yake kwa bidii, umakini na kuweka juhudi za dhati katika kuisaidia tume kushughulikia masuala ya utawala bora katika mazingira magumu sana.

Baada ya kutafakari kwa kina matukio ya sasa katika tume hiyo na kushauriana na familia yake na mawakili, Cherera alisema kwamba alikubali kukaa kwake katika tume hiyo hakustahili tena na hivyo akachagua kujiuzulu.Haya yanajiri baada ya  kamishna wa IEBC, Justus Nyang’aya kujiuzulu kutoka wadhifa wake Ijumaa wiki iliyopita.

Nyanga’aya na makamishna wengine watatu wanatuhumiwa kwa kujaribu kubadilisha matakwa ya wananchi katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

Wengine wawili ni Kamishna Irene Masit na Francis Wanderi.Matokeo manne yalikanushwa ambayo yalitangazwa na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukat

 

 

December 5, 2022