Wito umetolewa kwa wazazi kuwatunza wana wao vyema haswa wakati huu ambapo wako kwenye likizo ndefu. Huu ni wito wake naibu chifu wa Olashapani Purity Tompo.

Akizungumza ofisini mwake, Bi. Tompo amesema kuwa wasichana wengi wamepachikwa ujauzito katika eneo hilo wakiwa wamewatembelea jamaa zao akisema kuwa baadhi yao wanakeketwa kisiri jambo linalochangia kudorora kwa masomo ya mtoto wa kike eneo hilo.

Aidha chifu huyo ameyataka makanisa kushirikiana na serikali ili kuwakamata wanaokiuka haki za mtoto wa kike.

December 5, 2022