BY ISAYA BURUGU 22ND AUG 2023-Kizazaa kimeshuhudiwa leo katika kituo cha polisi cha Kerugoya baada ya makundi mawili hasimu kisiasa kukabiliana NA kupelekea mwakilishi kina mama  kaunti ya Kirinyaga Jane Njeri Maina akipata majeraha mabaya ya kichwa.

Njeri  ambaye ni wakili alikuwa ameandamana na mteja wake  ambaye ni MCA wa Bragwi  David Mathenge kwenda katka kituo hicho kuandikisha taarifa kuhusiana na madai ya kuharibiwa kwa muradi wa maji wa kaunti  katika kijiji cha Mukanduin wki iliyopita.Akiwahutubia wandishi habari baada ya kuandikisha taarifa,

Njeri amesema atamwakilisha MCA huyo  iwapo atafikishwa mahakamani.Ghazia zilianza wakati watu wanaoshukiwa kuwa wahuni  wanaosemekana kuegemea upande wa gavana  Anne Waiguru walipojitokeza na kuhitilafiana na kikao hicho cha wanahabari  na kuwashambulia wafuasi wa mwakilishi huyo wakike na MCA huyo.

Kundi la Zaidi ya vijana kumi lilirusha mawe walikokuwa wafuasi wawajumbe hao  na kuiba simu zao kabla ya kufurushwa.Awamu ya pili ya makabiliano yalitokea pale Njeri na Mathenge walipokuwa wakitembea katikabarabara za mji wa Kerugoya  ambapo kundi lingine la vijana lilianza kuwashambulia kwa mawe.

 

 

Share the love
August 22, 2023