William Ruto KRA

Rais William Ruto ametoa changamoto kwa mamlaka ya ukusanyaji wa ushuru nchini, akiitaka kuimarisha juhudi zake za kukusanya ushuru kwa kuwahusiaha wakenya na kuweka mazingira ya kupendeza kwa wakenya ili kuwahusisha kwa urahisi.

Akizungumza katika hafla ya kusherehekea siku ya walipa ushuru iliyoandaliwa katika chuo kikuu cha Kenyatta, Rais ameitaka KRA kutia bidii na kukusanya angalau shilingi Trilioni tatu kufikia mwisho wa mwaka ujao wa kifedha na kuhakikisha kuwa kipato hiki kinafikia mara mbili ya ushuru wa sasa kabla ya kukamilika kwa kipindi cha miaka 5 ijayo.


Zaidi ya hayo rais ameitaka KRA kukumbatia Teknolojia na kuiga mfano wa kampuni ya mawasiliano ya Safaricom ambayo imeweza kuwekeza pakubwa na kufanikiwa katika matumizi ya Teknolojia.

October 28, 2022