Elon Musk anunua Twitter

Bilionea Elon Musk amekuwa mmiliki mpya wa kampuni ya mtandao wa kijamii wa Twitter, na ameanza kazi kwa kuwaondoa wakurugenzi wakuu wa kampuni hiyo.

Watu walio karibu na kampuni hiyo wamearifu kuwa waliotimuliwa ni pamoja na mkurugenzi mkuu Parag Agrawal, mkuu wa kitengo cha fedha Ned Segal, na mkuu wa masuala ya sheria, Vijaya Gadde. Hata hivyo, Musk hakutoa ufafanuzi wa kutosha juu ya malengo makubwa aliyojiwekea ya kulibadilisha jukwaa hilo.

Baada ya kukamilisha ununuzi wa kampuni hiyo Musk alichapisha ujumbe usemao, the bird is freed (ndege ameachiwa huru) akiirejelea nembo ya Twitter, katika kile kinachotafsiriwa kama azma yake ya kupunguza vuzuizi katika maudhui yanayoweza kuwekwa kwenye mtadao huo.

October 28, 2022