Huku zoezi la kusambaza chakula cha msaada likiendelea katika maeneo mbalimbali kaunti ya Narok, onyo imetolewa kwa watu wanaouza chakula hicho kwa wakaazi wa maeneo yanayokabiliwa na baa la njaa. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa shehena ya chakula cha msaada, gavana wa Narok Patrick Ntutu amesema kuwa kuna baadhi ya watu wanaopanga kuuza chakula hicho kwa manufaa yao.

Ntutu ameeleza kuwa Narok imepokea na kusambaza magunia 3,200 ya kilo 50 za mchele na magunia 1,280 ya kilo 50 za maharage. Chakula hicho kimesambazwa katika maeneobunge ya  TransMara magharibi, TransMara mashariki, Emurua Dikir, Narok magharibi, Narok mashariki, Nairagie Enkare, Narok ya kati na Narok kusini.

October 28, 2022