Chama cha mawakili nchini LSK kimewaandikia barua polisi, kutaka taarifa kuhusu idadi ya watu waliokamatwa na kuzuiliwa wakati wa maandamano ya Azimio.

Pia inawataka polisi kuwapa stakabadhi zozote zinazohusiana na uchunguzi wa maiti na chanzo cha vifo vya waliofariki kutokana na maandamano hayo.Vile vile, LSK inataka kupewa majina ya watu waliouawa tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya serikali.

Chama hicho kimetaka taarifa hizo ziwasilishwe kwao ndani ya siku saba. Kupitia kwa mwenyekiti wake Erick Theuri, LSK ilisema itachukua taarifa hizo na kuzingatia hatua za kisheria dhidi ya polisi kuhusu ukiukaji wa haki na matumizi ya nguvu zisizofaa kwa waandamanaji.

August 3, 2023