BY ISAYA BURUGU,3RD AUG 2023-Serikali imedhibitisha  kuwa muradi wa sarafu kidigitali ya Worldcoin, ambayo oparesheni zake zimesitishwa  humu nchini haujasajiliwa kisheria nchini Kenya.

Kupitia taarifa ya Pamoja iliyotolewa na wizara za usalama wa ndani  sawa  na ile ya teknologia ya mawasiliano ya ICT ,imetoa ufichuzi huo  ikijibu swali lililoibuliwa na mbunge wa  Manyatta  John Mukunji  bungeni hiyo jana.

Kwa mjibu wa serikali ,kampuni hiyo ya kigeni ilikabidhi huduma zake za kukusanya data kwa kampuni ya humu nchini iliyotambuliwa kama Sense Marketing, iliyokuwa ikikusanya maelezo kutoka kwa wakenya  huku ikiwalipa shilingi alfu saba.

Mkuruygenzi mkuu wa idara ya upelelezi nchini DCI hiyo jana aliwanasa maafisa wawili  wa kampuni ya  Worldcoin  humu nchini  na sasa wanawasaidia makachero kwa uchunguzi kuhusu muundo na oparesheni za sarafu hiyo.

Wawili hao ni Emmanuel Otieno, anayesemekana kuwa mkuu wa oparesheni na  Rael Mwende ambaye ni meneja wa kampuni hiyo humu nchini.

 

 

 

August 3, 2023