Maafisa nane kati ya tisa wa kitengo cha SSU kilichovunjwa wamerudishwa rumande huku mmoja wao akiachiliwa kwa dhamana ya kima cha shilingi laki tano. Tisa hao walifikishwa katika mahakama ya kahawa mbele ya hakimu Diana Mochache ambapo mmoja wao aliweza kudhibitisha kuwa hakuwepo kazini wakati wa kutekelezwa kwa njama ya kuwateka nyara raia wawili wa India na dereva wao mkenya. Nane hao wataendelea kuzuiliwa kwa siku 21 zaidi ili kutoa nafasi ya kukamilika kwa uchunguzi.

November 10, 2022