BY ISAYA BURUGU ,19TH DEC 2022-Maafisa wa polisi wa DCI wamemkatama mwanname mmoja wa miaka 26 kuhusiana na jaribio la mauaji yam toto Juniour Sagini  kule marani kitutu chache kasikiani kaunti ya Kisii.Kwa mjibu wa polisi ni kwamba mwanamme huyo Alex Maina Ochogo ndie mshukiwa mkuu wa jaribio la maujai yam toto huyo mwenye umri wa miaka mitatu kwa kumngoa macho.OChogo anawasilishwa mahakamani huko kisii kukabiliana na kosa hilo la kujaribu kumua mtoto huyo.

Wakati huo huo Mama wa mtoto  Junior Sagini mwenye umri wa miaka 3  aliyevamiwa na macho yake kung’olewa  na watu wasiojulikana  huko Kisii anatarajiwa kufikishwa mahakamani hivi leo.

Mama huyo kwa jina Maureen Nyaboke,  alijitokeza kwa mara ya kwanza jana jumapili tangu kisa hicho kutokea .Kwa mjibu wa rekodi za polisi   ni kwamba      Nyaboke mwenye umri wa miaka 28  alimwacha mtoto huyo  pmoja na mtoto msichana  wa miaka saba   chini ya uangalizi wa babake na nyanyake.

Anaripotiwa kuenda kufanya kazi kama mhudumu wa baa eneo Nyamakoroto, kaunti ya Nyamira wakati kisa hicho cha kuhuzunisha kilipotokea jumatano wiki iliyopita.Ni mara ya kwanza mamake Sagini alikuwa akitembelea  hospitali ya macho ya Kisii  ambapo mtoto wake amekuwa amelazwa.

Wakati Nyaboke alipokuwa akijiandaa kuondoka hospitalini maafisa wa polisi walifika na kumtia mbaroni  na kumpeleka katika kituo cha polisi cha  Rioma kuhojiwa.Mama huyo amekesha korokoroni usiku wa leo huku akitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kumtelekeza mwanawe.

December 19, 2022