Muungano wa madaktari nchini KMPDU umetoa makataa ya siku thelathini kabla ya kuanza mgomo wa kitaifa.

Kulingana na katibu mkuu wa muungano huo Devji Atela, madaktari watashiriki mgomo huo kushinikiza serikali kuu na serikali za kaunti kutekeleza mkataba wa maafikiano wa 2017.

Atela ameeleza kuwa masuala yaliyoafikiwa kwenye mkataba huo kama vile kuongeza madaktari mshahara, kuwapandisha vyeo na kuhakikisha kuwa wana vifaa hitajika kazini hayajaafikiwa.

December 19, 2022