Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ameagiza kuhamishwa kwa maafisa wa polisi, maafisa wa KRA, wale wa KEBS pamoja na maafisa wa uhamiaji katika eneo la Isebania kaunti ya Migori.

Hatua hiyo imejiri baada ya watu watano kuuwawa kwa kupigwa risasi kufuatia makabiliano baina ya wakaazi na maafisa wa polisi.

Kindiki ameeleza kuwa serikali haitaendelea kuwahamisha maafisa wanaokikuka wajibu wao bali itawafuta kazi. Aidha amewakosoa wakaazi wa eneo hilo kwa kukivamia kituo cha polisi cha Isebania akisema kuwa walichochea vurugu.

Aliongeza kuwa Kama nchi, ni lazima tutatue kero zote kwa amani, haijalishi mtu amedhulumiwa kiasi gani huku akitoa wito kwa Wakenya wote kutochukua  sheria mkononi, kulipiza kisasi na uharibifu wa mali ili kutafuta haki.

Hali kadhalika amedokeza kuwa  hakuna askari polisi atakayehudumu katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitatu.

May 31, 2023