Mabawabu watatu mjini Migori waliuwawa usiku wa kuamkia leo na mwili wa mmoja wao kutupwa katika mto Migori. Maafisa wa polisi katika eneo hilo, walidhibitisha kupata miili ya watatu hao asubuhi ya leo, ikiwa na majeraha katika sehemu za shingo na Kichwa.

Aidha Bado haijabainika kilichosababisha tukio hilo la unyama, huku wananchi wakiielekeza kidole cha lawama kwa maafisa wa polisi, wakisema kwamba wamezembea katika kazi zao.

Wananchi hao sasa wanamtaka waziri wa usalama na utawala wa kitaifa Kithure Kindiki kuingilia kati na kuwakwamua kutoka kwa wahalifu hawa, ambao walitekeleza mauaji ya mlinzi mwingine mwezi Februari mwaka huu.

October 7, 2023