Mahakama ya leba imewaamuru marubani kurejea kazini kufikia kesho mwendo saa kumi na mbili alfajiri bila masharti yoyote. Mahakama hiyo iliwaita maafisa 11 wa KALPA baada ya kukataa kusitisha mgomo huo ambao umetajwa kuwa kinyume cha sheria.

Marubani hao ambao walifika mbele ya jaji Ann Mwaure mapema hii leo, waliitaka mahakama kuwapa siku saba ili wasuluhishe mgogoro wao na usimamizi wa shirika hilo ila ombi lao likatupiliwa mbali.

Aidha Jaji Mwaure vilevile ameliamuru shirika hilo la Kenya Airways kutowachukulia hatua za kinidhamu marubani walishiriki mgomo huo ambao umeingia siku ya nne.

November 8, 2022