Chief Justice

Idara ya mahakama inapania kuongeza muda wa kuhudumu kwa mahakama katika badhi ya miji humu nchini, ili kusaidia kupunguza mzigo na mrundiko wa kesi katika mahakama humu nchini.

Haya ni kwa mujibu wa Jaji mkuu nchini Bi Martha Koome ambaye amesema kwamba miji ya Nairobi na Mombasa ina uwezo wa kuwa na mahakama inayotoa huduma hadi saa za usiku, kuwawezesha wananchi Zaidi kupokea huduma za mahakama.

Akizungumza katika hafla ya kuwasilisha ripoti ya utendakazi wa mahakama humu nchini, jaji Mkuu pia ameeleza kuridhishwa na mipango iliyowekwa ya kuanzishwa kwa mahakama za kukabiliana na kesi za mizozo ya kijinsia.

November 4, 2022