Alfred mutua

Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Alfred Mutua ameahidi kushughulikia jinamizi la mizozo inayowakumba wafanyikazi wa Kenya wanaohangaika katika mataifa ya nje hasa mataifa ya uarabuni wanapoenda kutafuta ajira.

Akizungumza baada ya ziara yake katika taifa la Saudi Arabia, Waziri Mutua aliweka wazi kuwa maajenti wanaowapeleka wafanyikazi hawa katika mataifa pia wanachangia kuteseka kwa wakenya akiahidi kufanya uchunguzi wa kina na kufunga baadhi ya maajenti haw ana kufutlia mbali leseni za baadhi yao.

Waziri Mutua pia amesema kuwa hakuna raia yeyote wa humu nchini atakayeruhusiwa kufanya kazi katika taifa lingine pasi na kuafikia vigezo na matakwa yaliyowekwa kuanzia siku ya Jumatatu.

November 4, 2022