Kiongozi wa wengi bungeni Kimani Ichung’wa amemjibu Kinara wa azimio la umoja-one Kenya Raila Odinga kufuatia hotuba yake ya hapo jana. Akizungumza na waandishi wa habari, Ichung’wa amesema kuwa iwapo Odinga anayafahamu majina ya maafisa wa polisi waliohusika na mauaji ya wafanyakazi wa serikali basi anapaswa kuandikisha taarifa kwa idara ya DCI. Kuhusiana na suala la uchumi, Ichung’wa amedokeza kuwa bw. Odinga alichangia kuzorota kwa uchumi wa taifa hili akidai kuwa alitekeleza majukumu yake kama kiongozi wa upinzani.

 

November 4, 2022