Mahakama ya mazingira nchini imetupilia mbali kesi iliyokuwa ikipinga uamuzi wa serikali kuruhusu uagizaji na upandaji wa vyakula vya GMO.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Oscar Angote amesema kuwa hakuna ushahidi wa kuonyesha madhara ya vyakula hivyo kwa mazingira au afya ya binadamu huku akishikilia kuwa umma ulihusishwa kikamilifu kuhusiana na suala hilo la uagizaji wa vyakula hivyo.

Mwezi Oktoba mwaka 2022, serikali iliondoa marufuku ya muongo mmoja dhidi ya mazao ya GMO ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa chakula kufuatia ukame mbaya zaidi uliolikumba eneo la Pembe ya Afrika katika miaka 40.

Mwanasheria Paul Mwangi aliwasilisha kesi mahakamani, akisema uamuzi huo ni kinyume cha katiba kwa sababu kulikuwa na wasiwasi ju ya usalama wa mazao hayo.

Share the love
October 12, 2023