BY ISAYA BURUGU,7TH MARCH,2023-Naibu kamishna wa Narok kusini Felix Kisalu ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Narok kutoa mafunzo kwa wakulima katika maeneo ya nyanjani kama njia moja ya kuboresha mavuno  msimu huu wa upanzi.

Akizungumza katika eneo la Sogoo Narok kusini, Kisalu amesema kuna haja  ya kuwafunza wakulima tecknologia ya kisasa kufuatia tatizo la mabadiliko ya tabia nchi.

Kisalu amesema serikali ya kitaifa itashirikiana kwa karibu na serikali ya kaunti ya Narok kuwasaidia wakulima.

wakati uo huo Kisalu amesema kwa mara nyingi wakulima wamekosa ujuzi wa upanzi sawa na utabiri hali ya anga ili waweze kufanikiwa katika  upanzi na kupata matokeo bora hatua ambayo imepelekea mapato duni eneo hilo.

 

 

March 7, 2023