BY ISAYA BURUGU 9TH JAN,2022-Makamishna saba wa Tume ya Ugavi wa Mapato walioteuliwa wameapishwa rasmi leo kuanza jukumu lao. Hii ni baada ya Bunge la Kitaifa kuwaidhinisha makamishna hao saba mnamo Desemba 8, 2022, baada ya kufika mbele ya Kamati ya Bunge ya Fedha na Mipango ya Kitaifa ili kupigwa msasa.

Hafla hiyo imeongozwa na jaji mkuu Martha Koome katika majengo ya mahakama ya juu. Saba hao ni pamoja na aliyekuwa Mwakilishi wa kina mama kaunti ya Wajir Fatuma Gedi, George Jalang’o Midiwo na Wilfred Koitamet Olekina kutoka Chama cha Wachache katika Bunge la kitaifa.

Chama cha Wengi bungeni kwa upande mwingine kiliwachagua Benedict Muasya Mutiso, Jonas Misto Vincent, Isabel Nyambura Waiyaki na Hadija Nganyi Juma.

 

January 9, 2023