BY ISAYA BURUGU  9TH JAN 2022-Mwanume mwenye umri wa miaka 40 anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Narok kwa tuhuma ya kukiuka haki za watoto kwa kumoa msichana wa mwenyeumri wa miaka 7 ambaye sasa ana miaka 12.Inaarifiwa kwamba muuguzi mmoja katika hospitali ya rufaa ya Narok aliwajulisha maafisa wa polisi kuhusiana na kisa hicho msichana huyo alipofikishwa hospitalini kujifungua. Msichana huyo alilazimishwa kuingia kwenye ndoa ya mapema na babake baada ya kupashwa tohara akiwa na umri wa miaka saba.Aidha kwa mujibu wa muuguzi Kaliej Kimani anayefanya kazi katika hospitali hiyo ya rufaa, msichana huyo alifanyiwa upasuaji ila mtoto akafa kutokana na matatizo ya kiafya.

 

Kwingineko  Maafisa wa polisi Narok kusini wannachunguza kisa ambapo mwili wa mwanamme wa umri wa makamu  umepatikana  katika bwawa  moja eneo la majimoto  Narosura.Kwa mjibu wa maafisa wa polisi mwanamme huyo  aliyetambuliwa kama  Tom Leintoi  amekuwa na tatizo la kiakili.Nduguye marehemu  Peter Leintoi  anasema marehemu ambaye ni kiongozi wa rika la  ilmeshuki alipotea nyumbani  bbada ya kulalamikia maumivu na baadaye mwili wake kupatikana katika bwawa hilo.Mwili wa mwendazake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia  maiti  katika hospitali ya rufaa mjini Narok.

 

 

 

 

January 9, 2023