Washukiwa watano wa  mauaji ya mwanaharakati wa ubasha Edwin Chiloba wataendelea kuzuiliwa kwa wiki tatu zaidi ili kutoa nafasi ya kukamilika kwa uchunguzi.

Tano hao ambapo watatu kati yao hawajahitimu umri wa miaka 18 walifikishwa katika mahakama ya Eldoret. Jacktone Odhiambo ambaye ni mshukiwa mkuu anatuhumiwa kumuua  Chiloba aliyepia mwanamitindo.

Aidha Polisi walifanikiwa kulinasa gari linaloshukiwa  kutumiwa  kuubeba mwili  wa Chiloba  ambao baadaye ulipatikana umetupwa kando ya barabara.

kikosi cha wachunguzi wa mauaji tatanishi  wanatarajiwa kusafiri hadi Eldoret kusaidia katika uchunguzi.Chiloba alipatikana ameuwawa  ijumaa iliyopita na mwili wake kuwekwa ndani ya sanduku la nguo na kutupwa  huko Kipkaren viungani mwa mji wa  Eldoret  kaunti ya  Uasin Gishu .O

dhiambo alikiri kumuua mwana mitindohuyo  kwa madai kuwa  alikuwa na mpenzi mwingine.

January 9, 2023