Watoto watano waliozaliwa Pamoja katika hospitali ya Nakuru Level IV siku ya jana wameaga dunia.

Watoto hao wamedhibitishwa kuaga dunia baada ya kuzaliwa kabla ya wakati unaofaa, matabibu wakieleza kuwa viungo vyao vya mwili havikuwa vimekomaa, jambo ambalo limesababisha kuaga kwao walipokuwa wakiendelea kupokea huduma za uangalizi na madaktari katika hospitali hiyo.

Simon Ndungu Kinyanjui aliye na umri wa miaka 28 na mkewe Margaret Wangui aliye na umri wa miaka 25, walipata watoto hawa ambao walikuwa na wiki 25 pekee, na hivyo kulazimu matabibu kuwaweka chini ya uangalizi wa kina huku wakizidi kutathmini jinsi wanaendelea.

Taarifa za kuaga dunia zimedhibitishwa na jamaa ya wazazi hawa mapema leo, wakisema kwamba watoto wawili waliaga dunia kwanza, kabla ya waliosalia pia kudhibitishwa kuwa wameaga dunia. .

February 2, 2023